January 29, 2015

RAIS WA CAF, ISSA HAYATOU (KULIA) AKIWA NA RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI.

Mo van der Mhando, China
UNAWEZA kunishangaa lakini kwangu haya ninaweza kuyaita ni maajabu ya dunia kwenye karne hii ya 21 na moja kwenye soka la Africa.


Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limepitisha uamuzi wa droo ya timu mbili tu, ilipangwa kufanyika jana jioni ili kuangalia timu ipi kati ya Mali au Guinea itafuze kucheza robo fainali ya Kombe la Mataifa Afrika (Caf).
Hali hiyo inatokana na timu hizo kulingana kila kitu katika kundi D ambalo Ghana ndiyo kinara. Sasa Guinea na Mali zinagombea hiyo nafasi moja ya kwenda robo fainali.

Nimeambiwa hata Fifa hutumia mfumo huo, lakini sihawahi kusikia hata mara moja kwa kuwa hauna tofauti hata kidogo na ule wa kurusha shilingi enzi hizo.

Kama mipira miwili itawekwa na kuchagua mshindi mmoja, kuna tofauti gani na yale mambo ya enzi zile ya kurusha shilingi?

Dunia inatushangaa Waafrika kwa hili hakuna ambaye alitarajia kukutana na kituko kama hiki kwenye karne.

Timu hizo zote mbili hazijashinda mchezo hata mmoja wa kundi hilo zaidi ya kutoka sare ya bao moja kwa moja kwenye michezo yao yote mitatu na sasa Caf wanaota njia pekee ya kumpata mshindi eti ni kuchagua mipira kama vile wanapanga makundi na mimi naita ni sawa na urushaji wa shilingi.

Aibu ilioje kwa soka la Africa huwezi kumueleza mtu upuuzi huu akakuelewa kwa haraka haraka zaidi ya hao wenyewe Caf. Mimi naona si sawa, naona hii ni sawa na kuidhulumu timu moja na kuipendelea nyingine tena bila ya woga.


Najiuliza hivi kweli Caf walikosa kabisa njia nyingine sahihi ya kupata mshindi wa mchezo huo kuliko kurusha shilingi? Wadau wengi wanajiuliza kwanini wasipige hata penalti ilikuweza kumpata mshindi wa mchezo huo na hiyo nadhani ndio ingekuwa njia sahihi na isingeleta malalamiko.

Hata kocha wa timu ya Taifa ya Mali, Henryk Kasperczak raia wa Poland amenukuliwa akisema hajapendezwa na  mtindo wanaotaka kutumia Caf kumpata mshindi na kusema hana hakika kama walikosa njia sahihi ya kumpata.
Kauli ya kocha huyo inaonyesha wakati jana Mali na Guinea wakienda kwenye hatua hiyo ya kuteuliwa kusonga mbele, hakuna aliyekuwa ameridhika na hata mmoja akishinda, mwingine atakuwa kaonewa.

Hapa lazima tuwe wawazi na tuseme kweli viongozi wengi wa soka la Afrika wanafanya kazi kwa mazoea au niseme kwa kukariri sana na ndio maana wakaja na wazo jepesi kabisa kama hili huku wakidhani ni njia sahihi ya kupata mshindi.

Issa Hayatou na wenzie hapa wamechamsha kweli kweli na hilo linajieleza wazi ni kutokana na udikteta wao wa kwenye soka la Afrika na kutokutaka kupokea mawazo mapya na ndiyo maana hata wakaweka sheria eti mtu hawezi kugombea Urais wa Caf kama sio mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama hicho.

Wakati wao wakija na njia hiyo ambayo inaacha utata mkubwa, wenzetu wanazidi kupiga hatua na mfano mzuri ni mechi za Kombe la FA nchini England. 

Mechi ya kwanza kati ya Liverpool iliisha kwa sare ya bao 1-1, mechi ya pili ikaisha 0-0 na bado dakika 120 zikaongezwa kwa kuwa ni sheria iliyoboreshwa. Wametoa faida ya bao la ugenini katika sare. Caf wako wapi?



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic