Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kuliomba Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kumchukulia hatua straika wa Yanga, Amissi Tambwe kutokana na kumpiga
kibao beki wa Ruvu Shooting, George Michael, uongozi wa Yanga umeibuka na
kujibu mapigo.
Tambwe na beki huyo waliingia kwenye vita kali
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa katika Uwanja wa Taifa huku
awali Tambwe akilalamika kuwa beki huyo alimkaba koo lakini baadaye ikafahamika
kuwa naye alimpiga kibao.
Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha,
ameishangaa kauli ya Hans Poppe kwa kile alichosema anaingilia mambo
yasiyomhusu huku akihoji kama siku hizi amekuwa msemaji wa wanajeshi hao, kazi
ambayo ni ya Masau Bwire.
“Ki
ukweli ilinishangaza sana kusikia kauli ya kiongozi wa timu isiyohusika katika
tukio kulisemea kuwa Tambwe anatakiwa kufungiwa, ni maajabu sana. Mimi binafsi
sijawahi kumsikia kiongozi yeyote wa Yanga akizungumzia timu nyingine, labda
iwe na mechi na timu yake na huo ndiyo weledi kitaaluma (professionalism).
“Haiingii akilini hata chembe kusikia kiongozi
wa Simba anaibuka na kuzungumzia mchezo usiomhusu hata kidogo, labda aweke wazi
kama siku hizi ameajiriwa na Ruvu ili tujue moja,” alisema Dk Tiboroha.
Sakata hilo liliibuliwa na gazeti kiongozi la
michezo nchini, Championi lililochapisha picha iliyomuonyesha Michael akimpiga
kabali Tambwe huku akivuja damu mdomoni na baadaye kuonyesha nyingine fowadi
huyo akijibu mapingo kwa kumpiga beki huyo kofi.
0 COMMENTS:
Post a Comment