February 28, 2015


Wanachama na viongozi wa Klabu ya Simba, wanatarajia kukutana kesho Jumapili saa nne asubuhi katika mkutano mkuu utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar ili kuweka mambo sawa.


Simba ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 20 ikiwa imefungwa mabao 12 na kufunga 15 ikiwa imetoa sare michezo nane na kupoteza  michezo mitatu na kushinda minne katika ligi.

Rais wa Simba, Evans Aveva, amefunguka kuwa, ajenda watakayokwenda kuijadili katika mkutano huo ni kuhusu mwenendo wa timu hiyo katika ligi kwa lengo la kuikwamua timu ili iwe na kiwango kizuri katika mechi zinazofuata.

Alisema mkutano huo utakuwa wa kawaida na watahakikisha wanatoa nafasi kwa kila mtu kutoa ya moyoni kwa lengo la kujenga.

 “Mkutano wetu upo palepale na unatarajia kufanyika saa nne asubuhi Jumapili katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay ambapo ajenda itakuwa moja tu ya kujadili juu ya mwenendo wa timu yetu kwenye ligi.

“Tunahitaji kuijenga timu ili iweze kuwa vizuri, hivyo ni wajibu wa wanachama wote kujitokeza na kujadili suala hilo kwa kina na kuleta umoja,” alisema Aveva.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic