February 1, 2015


Majirani wa Tanzania, DR Congo wamewagalagaza majirani zao Congo, maarufu kama Congo Brazzaville kwa kuwachapa mabao 4-2 licha kuwa walianza kwa kufungwa.


DR Congo sasa wamefuzu hadi nusu fainali ya michuano ya Afcon.


Congo ambao walifuzu baada ya Caf kuwaengua Rwanda, walitangulia na kufunga mabao 2-0 wakiwaacha nyuma DR Congo ambao baadaye walipambana vilivyo na kufunga mabao manne.


Kipindi cha pili kilionekana kuwa mali ya DR Congo na washambuliaji wake Thievy Bifouma aliyefunga mabao mawili, Dieumerci Mbokani na wenzake wakionekana kuwapa wakati mgumu majirani na wapinzani wao wakubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic