February 1, 2015













MPIRA UMEKWISHAA
Dk 90+3 Chachala analambwa kadi ya njano kwa kwa kumpiga teke Msuva.


Dk 90, Ernest Mwalupani anapigwa kadi ya pili ya njano inayozaa nyekundu.
Dk 83, Tambwe anapata nafasi nzuri lakini anapiga shuti mtoto 

Dk 80 Tegete anaingia kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa 
Dk 81, Yanga wanafanya shambulizi kali baada ya pasi nzuri ya Tambwe, lakini mabeki wa Ndanda wanaondoa hatari.
Dk 78, Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa mara mbili mashuti ya washambuliaji Ndanda


Dk 77, Mrwanda yeye na lango anashindwa kufunga
Dk 72 Isihaka anaingia ndani ya boksi, anapiga shuti lakini Cannavaro anaokoa.

Dk 70 Ndanda wanamuingiza Shukuru Chachala badala ya Ngalema aliyeumia.
Dk 67, Tambwe anapiga kichwa saafi lakini mpira unapita juu ya lango.


Dk 63 Ndanda inamuingiza Rajab Isihaka kuchukua nafasi ya Masoud Ally.
Dk 62 Ngalema anaumia wakati akijaribu kumkaba Mrwanda, anatolewa nje.
Dk 60 Yanga inamtoa Sherman na nafasi yake inachukuliwa na Amissi Tambwe.

Dk 56 Mwamuzi Martin Saanya anamlamba Sherman kadi ya njano kwa kujiangusha ndani ya eneo la hatari.




Dk 51 Sherman anapiga shuti ndani ya 12 ya Ndanda lakini inagongwa mwamba na kutoka nje.
Dk 47 Mrwanda anapiga mpira wa faulo lakini unaishia mikononi mwa Mweta.

Dk 46 Massawe anapiga shuti lakini Bharthez anadaka.
MAPUMZIKO:

Dk 44 Masoud Ally anapiga shuti kali baada ya kugeuka lakini Barthez anadaka
Dk 42 Mweta anatoka na kugongana na Sherman. Sasa kipa huyo anatibiwa na mpira ni kona itaelekezwa lango la Ndanda, kona inapigwa, goak kick.


Dk 36 Sherman anapiga kichwa safi lakini kipa Mweta anaokoa kwa ustadi.


Dk 35 Zabron Raymond analambwa kadi ya njano baada ya kumwangusha Ngassa katikati ya uwanja.

Dk 27, Yanga inapata kona ikiwa ni ya pili katika mchezo huu, anaichonga Msuva lakini Cannavaro akiwa analiangalia goli la Ndanda, anapaisha.

Dk 22, Mweta tena anafanya kazi ya ziada kuruka na kukoa mpira wa kichwa wa Sherman baada ya krosi safi ya Msuva.

Dk 21, Ngassa anatoa pasi nzuri kwa Sherman lakini kipa Mweta anatoka na kuokoa mpra huo


Dk 14 hadi 20, zaidi mpira unachezwa katikati na hakuna mashambulizi makali zaidi.

Dk 13 Sherman akiwa ndani ya 18, anapiga shuti mtoto kabisa.

Dk 11, Ngassa naye anashindwa kuunganisha krosi safi Juma Abdul
Dk 8, Msuva anapewa pasi nzuri na Ngassa lakini anashindwa kufunga na kumpasia kipa.
Dk 4 Samir Mbonde anakosa bao la wazi baada ya kushindwa kupiga kichwa hatua tatu kutoka langoni mwa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic