February 27, 2015

MPIRA UMEKWISHAAAAAA.....
DK 4 ZAONGEZWA
Dk 89, pasi nzuri ya Tambwe lakini Msuva anashindwa kufunga
Dk 87, anaingia Sherman Kpah kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa

GOOOOOO Dk 85, BDF wanafunga la pili kupitia Kumbulani ambaye alipiga mpira, ukagonga mwamba. Ukamrudia na Yondani na Cannavaro kushindwa kuokoa, akapiga bao.

Dk 82 Oscar Joshua naye analambwa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda
Dk 81 Yangaw anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliokuwa unajaa wavuni nakuwa kona isiyo na manufaa.


Dk 78&80, BDF ndiyo wanaonekana kumiliki mpira zaidi. Sasa wanapata faulo kwa Barthez kukosea
Dk 77, Mastara anapiga kichwa kizuri lakini Barthez anatulia na kudaka vizuri
Dk 76, Msuva anapokea pasi ya kisigono ya Ngassa na kupiga shuti kali linalopaa juu ya lango

Dk 75 Kabelo wa BDF naye analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Niyonzima
KADI NYEKUNDU Dk 72 Mrwanda anapigwa kadi ya pili ya njano na kuzaa kadi nyekundu.


Dk 69,  Ngassa anapiga shuti jingine kali, lakini kipa analala na kuudaka kwa ufundi mkubwa

Dk 62, Nzombe anapiga shuti jingine, lakini Cannavaro anaweka kichwa na kuokoa mpira huo
Dk 58, BDF wanafanya shambulizi jingine kali, lakini Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa.
Dk49 BDf wanasawazisha bao kupitia Msimonyane
BDF WANAFANIKIWA KUPATA BAO NA MATOKEO SASA NI BAO
KIPINDI CHA PILI KINAONEKANA KUWA KUNA MABADILIKO ZAIDI KWA UCHEZAJI KWA BDF AMBAO WANASHAMBULIA MFULULIZO.

MAPUMZIKO:

Dk 45 Yanga wanajipanga na kushambulia vizuri na krosi safi ya Mrwanda inamfikia Tambwe, anapiga kichwa safi, kinagonga mwamba na kutoka nje.

Dk 42, Juma Abdul anawapangua mabeki wa BDF, anapiga shuti lakini linaokolewa.


Dk 33, BDF wanaingiza mzuri ndani ya lango la Yanga, lakini kazi nzuri ya Barthez anatulia saaafi.


GOOOOOOOO Dk 29, Ngassa anaifungia Yanga bao safi kwa kichwa cha kuchupa baada ya basi nzuri ya Amissi Tambwe aliyeuwahi mpira alioutema kipa wa BDF.

Dk 22 BDF wanafanya shambulizi kali lakini mara mbili mabeki wa Yanga wanafanya kazi ya siada kuokoa.
KADI NYEKUNDU Dk 20 Othusitse Mpharithe analabwa kadi  ya nyekundi baada ya kumchezea rafu mbaya Simon Msuva ambaye sasa anatibiwa.

Dk 17, kadi ya kwanza ya njano, Gaolaolwe wa BDF anapigwa kadi kwa kumuangusha Juma Abdul


Dk 15, Mrwanda anapoteza nafasi nyingine kwa Yanga kwa kupiga shuti linalopita juu ya lango

Dk 14, shambulizi la kwanza kali la Seaakanyange wa BDF, anapiga shuti kali linapita juu ya lango.
Dk 12, Yanga wanafanya shambulizi kali, shuti la Mrwanda na Msuva, yote yanaokolewa
DK 11 Yanga wanapata faulo, anapiga Mrwanda inaokolewa na kuwa kona, lakini haina faida
DK 6, Yanga wanapata kona ya kwanza, lakini inakuwa haina madhara katika lango la BDF.
Dk 4, Ngassa anabaki yeye na kipa baada ya beki kuanguka, lakini anapiga mpira nje

Dk 1, Ngassa anapiga krosi lakini kidogo tu umfikie Tambwe kipa anawahi kuudaka.

Kikosi kilichoanza:

Barthez
Juma Abdul 
Oscar
Cannavaro
Yondani
Twite
Msuva
Niyonzima
Tambwe
Ngasa

Mrwanda



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic