February 27, 2015


Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe licha ya kuwa gumzo kubwa baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya BDF XI bado anaendelea kuwa na rekodi ya mchezaji pekee wa Yanga anayeujua vizuri Uwanja wa Lobatse utakaotumika kwa mechi ya leo.


BDF inaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Lobatse ulio kilomita 70 kutoka jijini hapa na Tambwe atacheza kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo miezi kadhaa iliyopita wakati timu yake ya taifa ya Burundi kulala kwa bao 1-0 na kung’olewa katika kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

Mechi hiyo kuwania kucheza Afcon ilipigwa Juni Mosi, 2014 na Burundi ikalala kwa bao hilo huku Tambwe akishindwa kutikisa nyavu za Waswana hao.

Julai Mosi, 2014, Botswana ikacheza mechi kirafiki dhidi ya Tanzania na kuichapa mabao 4-2, safari hii mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Taifa ulio hapa katika Jiji la Gaborone.

Kwa Tambwe, itakuwa ni mara ya nne kukutana na timu za Botswana ndani ya miezi saba. Mara ya kwanza walipotoka sare ya bila kufungana mjini Bujumbura, halafu wakalala kwa bao 1-0 huko Lobatse.


Mara ya tatu ni jijini Dar, safari hii akiichezea Yanga na kufanikiwa kufunga mabao yote katika ushindi wa 2-0. Swali, leo ataendelea kuonyesha sasa anawajulia Waswana?

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic