February 28, 2015


Kesho itakuwa siku nyingine ya kujiuliza maswali kwa Arsene Wenger wakati kikosi chake cha Arsenal kitakaposhuka dimba katika mchezo mgumu wa Ligi Kuu England.


Arsenal vs Everton
Baada ya kula kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa AS Monaco, Arsenal watarejea tena kwenye Uwanja wa Emirates, kesho wakitarajia kufanya maajabu kwenye Ligi Kuu ya England.

Vijana wa Kocha Wenger, wanaweza kupata mapokezi mabaya kutokana na kiwango kibovu ambacho walionyesha kwenye mechi hiyo ya Jumatano iliyopita.

Ushindi tu ndiyo unaweza kuwafanya wakaendelea kuwa na kasi nzuri, kwani wanaonekana kupishana kwa pointi tatu tu na Liverpool ambao wapo nafasi ya sita.

Arsenal wanafahamu kuwa pamoja na kwamba Everton msimu huu wanasuasua, bado wanaweza kufanya maajabu kama walivyofanya kwenye mchezo wa kwanza ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Katika mchezo huo, Arsenal walilazimika kusawazisha baada ya kutanguliwa hali ambayo inaweza kuwapa hofu kubwa vijana hao wa London hiyo kesho.


Arsenal wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye michezo kadhaa iliyopita ambapo wameweza kutoka katika nafasi ya saba hadi kutua kwenye tatu bora.

Everton kwa sasa wapo katika nafasi ya 12, wakiwa wameshinda mechi sita tu kati ya 26 na wanajua kuwa kupoteza mchezo wa leo ni jambo baya sana kwao na wakati wowote wanaweza kusogelea kwenye mstari wa kushuka daraja.

Taarifa zinasema kuwa huu unaweza kuwa mchezo wa mwisho kwa kocha wa timu hiyo, Roberto Martinez, endapo watapoteza.  

Uso kwa uso
2014/2015 :   Everton 2 - 2 Arsenal
2013/2014:  Everton  3 – 0  Arsenal

2013/2014:    Arsenal    4 – 1  Everton

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic