February 26, 2015

BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA WAKIWA KWENYE UWANJA WA LOBATSE NCHINI BOTSWANA IKIWA NI BAADA YA KUMALIZA MAZOEZI, LEO.

Uongozi wa Yanga umesema umeukubali Uwanja wa Lobatse kwamba uko safi na unastahili kuchezewa pambano la kimataifa.


Yanga inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Lobatse mjini  Lobatse kuivaa BDF katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho, kesho.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema uwanja huo una vigezo vyote na wanaamini watacheza vizuri.

“Ni uwanja mzuri na wote tumeuona, baada ya mazoezi kila kitu kimekwenda vizuri na kila mmoja wetu ameridhika na uwanja.

“Hatuwezi kuwa malalamiko yoyote kuhusu uwanja, hadi sasa tunachosubiri ni mechi tu,” alisema.


Uwanja wa Lobatse, uko kilomita 70 kutoka jijini Gaborone ambao ni mji mkubwa kuliko yote nchini Botswana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic