March 5, 2015

IBRA AJIBU 'KADABRA' (KUSHOTO) AKIWANIA MPIRA NA MOHAMMED HUSSEIN 'TSHABALALA' KATIKA MAZOEZI YA SIMBA MJINI ZANZIBAR.
Kocha Goran Kopunovic wa Simba amesema mmoja wa wachezaji wake walio tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Yanga, Jumapili ni mshambuliaji kinda, Ibrahim Ajib ‘Kadabra’.


Kinda huyo alifunga mabao matatu 'hat trick' katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu Bara wakati Simba ilipoitwanga Prisons kwa mabao 5-0.

Kopunovic amesema Ajib amekuwa akijifua vizuri na wenzake na anafurahi kuona kikosi ni kipana.

“Kikosi kinakuwa kipana kama wachezaji wote wako fiti, unakuwa na nafasi ya kuchagua,” alisema kocha huyo raia wa Serbia.

“Matumaini ni makubwa kwa kuwa vijana furaha na wako tayari kwa ajili ya kupambana hiyo Jumapili. Tunazihitaji sana pointi tatu.”


Simba imeweka kambi Zanzibar kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya watani wake Yanga ambao wameweka kambi mjini Bagamoyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic