March 29, 2015


Chelsea sasa imeamua, iko katika mipango ya kumnasa kiungo Gareth Bale na imetenga pauni milioni 75.


Iwapo itakubaliana na Real Madrid kumnasa Bale kwa kitita hicho itakuwa ni rekodi mpya ya usajili nchini England.

Taarifa kupitia gazeti la Dailymail la Uingereza zimeeleza kuwa Real Madrid tayari wana taarifa hizo za Chelsea lakini wanaona angalau Bale abaki msimu mmoja zaidi.

Bale alitua Madrid kwa kitita cha pauni milioni 86 akitokea Tottenham na kumfanya awe mchezaji ghali zaidi duniani.


Raia huyo wa Wales, tayari ameanza kuonyesha cheche zake akiwa na Madrid na jana aliifungia timu yake ya taifa mabao mawili wakati ikiichapa Esrael kwa mabao 3-0 katika mechi ya kuwania kucheza michuano ya Ulaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic