March 4, 2015

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ameamua kuwapumzisha wachezaji wake kesho.

Wachezaji wa Simba watafanya mazoezi kesho jioni baada ya mazoezi makali ya leo visiwani Zanzibar.
 
KIKOSI CHA SIMBA KIKIJIFUA LEO MJINI ZANZIBAR
Kopunovic amesema mapumziko ya asubuhi na baada ya hapo wataendelea kama kawa jioni.


“Mazoezi yalikuwa makali na wachezaji wamefanya vizuri. Inatia moyo na matumaini, watapumzika asubuhi halafu tutaendelea na ratiba jioni,” alisema.
 
BAADHI YA WACHEZAJI WA SIMBA KATIKA MAZOEZI YA LEO MJINI ZANZIBAR
Wakati wa mazoezi hayo, wachezaji wa Simba walionekana kufanya kwa juhudi kubwa, tena wakijiamini.


Simba iko kisiwani Unguja kujiandaa na mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, Jumapili ijayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic