March 31, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesisitiza hata kama iko ugenini, Simba inalazimisha kushinda dhidi ya Kagera Sugar.

Kocha huyo Mserbia amesema mechi hiyo ya wikiendi itakuwa ngumu kwao kutokana na ubora, lakini suala la ushindi ni muhimu.


“Tunajua Kagera ni timu nzuri, lakini katika ligi hii kumbuka hakuna timu dhaifu.
 
“Ila kuna timu kongwe na timu imara zaidi. Sisi tunachoangalia ni kufanya vizuri na kushinda.

“Tutaanza safari ya kwenda Kagera tukiwa na lengo moja tu, kushinda mechi na kurudi na pointi tatu,” alisisitiza MSerbia huyo.

Simba imekuwa ikiendelea kujifua kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic