March 31, 2015



Mashabiki mbalimbali wa klabu ya Yanga wanaanza safari leo kuifuata FC Platinum ya Zimbabwe.

Yanga itashuka dimbani katika ardhi ya Zimbabwe kuivaa timu hiyo katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho baada ya kuwa imeshinda 5-1 katika mechi ya kwanza jijini Dar.

Mashabiki hao kwa kutumia basi dogo aina ya Toyota Coaster watapitia Mbeya, Tunduma tayari kwa ajili ya kwenda kuishangilia Yanga katika mechi itakayopigwa Jumamosi.


Yanga inatarajia kuondoka kesho kwa ndege ya kukodi ya serikali, tayari kuwavaa FC Plutinum.


Pamoja na Yanga kuwa imeshinda kwa mabao 5-1, bado mechi hiyo inaonekana itakuwa ni ya ushindani mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic