March 2, 2015

Kocha Jose Mourinho aliwazuia wachezaji wake kuangalia mechi ya Ligi Kuu England kati ya Liverpool dhidi ya Manchester City.

Mechi hiyo ilikuwa kivutio kwa watu wote wa Chelsea, kwa kuwa walitamani kuona Liverpool inashinda ili kuendelea kuipa Chelsea nafasi ya kung’ang’ania kileleni.

Kweli Liverpool ilishinda mabao 2-1 lakini hakuna aliyeishuhudia kwa wachezaji na memba wote wa benchi la ufundi kwa kuwa Mourinho aliagiza chaneli zote zinazoonyesha mpira kuzimwa katika vyumba vya wachezaji.

Wachezaji wa Chelsea walikuwa hotelini katika maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Capital One.

"Kulikuwa na mchezo muhimu mbele yetu. Mechi ya City ilikuwa muhimu kwetu, hivyo ingewachanganya wachezaji,” alisema Mourinho.

"Kulikuwa pia kuna mechi ya Man United, sasa wako nafasi ya tatu. Usisahau wako katika vita ya kuwania ubingwa.

“Niliwaambia wachezaji kwamba nisingependa presha au kuona wanakufa nguvu kama City itafunga bao la ushindi mwishoni.


“Nilitaka akili yote ibaki katika mechi dhidi ya Spurs iliyokuwa mbele yetu,” alisema Mourinho ambaye alimzuia dereva wa basi kuwasha runinga wakiwa njiani wanakwenda uwanjani kuivaa Spurs.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic