March 22, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema hata haelewi mechi ya leo itachezwa vipi.



Kopunovic raia wa Serbia ameingia hofu ya mvua kama ilivyokuwa kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm jana kabla ya kuivaa Mgambo mjini Tanga.

"Mvua ni kubwa kama unavyoona, hata hali ya uwanja sijui itakuwaje. Lakini sisi tuko tayari.

"Tayari tumeanza safari ya kwenda uwanjani, tutaona huko itakavyokuwa," alisema.

Simba inatarajia kushuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kuivaa Ruvu Shooting.

Hata hivyo, mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam sasa imekuwa ikiongeza hofu kama mechi hiyo itakuwepo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic