March 30, 2015


Kumekuwa na taarifa kiungo nyota, Raheem Sterling hatakubali kusainik mkataba mpya na klabu yake ya Liverpool pamoja na kuwa imeongeza dau kubwa.


Liverpool iko katika hatua za mwisho kutaka kumsainisha mkataba mpya ikiwa imeongeza kitita cha pauni 180,000 ambacho atakuwa analipwa kwa wiki.

Lakini taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa Sterling zinaeleza hatasaini.

Hali hiyo kidogo inaonekana kuwachanganya Liverpool, lakini uongozi wake umeendelea kusisitiza una imani ataisaini.


Unachofanya sasa uongozi huo wa Liverpool ni kuendelea kumsubiri hadi atakaporejea kutoka majukumu ya timu ya taifa ya England ili kufanya naye mazungumzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic