March 28, 2015



Pamoja na Mrisho Ngassa kusema huu ndiyo msimu wake wa mwisho kuichezea Yanga, uongozi wa timu hiyo umesema hauna mpango wa kuachana na winga huyo na utahakikisha anabaki katika kikosi chao.


Mapema wiki hii, Ngassa amenukuliwa akisema mwishoni mwa msimu ndiyo mwisho wake Yanga na sasa anatakiwa na timu zikiwemo za Afrika Kusini, DR Congo na Qatar.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amesema: “Msione tupo kimya licha ya Ngassa kutamka vitu vingi, bado tuna mpango wa kukaa naye meza moja ili kujadili mkataba mpya.

“Hatujakata tamaa ya kumbakiza kwa kauli alizotoa za kutaka kuondoka, lengo letu tuwe naye kwani ana mchango mkubwa kwenye timu.”

Mkataba wa Ngassa na Yanga unaisha mwisho wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara lakini amekuwa hana furaha na klabu hiyo kutokana na deni la Sh milioni 45 analodaiwa na benki moja ambalo anadai klabu yake imekiuka makubaliano ya kumlipia.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic