March 29, 2015

MOJA YA NDEGE ZINAZOMILIKIWA NA SERIKALI YA TANZANIA.

Yanga inatarajiwa kwenda Zimbabwe Ijumaa, tayari kuivaa FC Platinum.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kufanya safari yao ya Zimbabwe kwa kutumia ndege ya serikali.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza timu hiyo itasafiri na ndege hiyo baada ya Yanga kufanikiwa kupata kibali.

Uamuzi wa kupanda ndege ya serikali ni kupunguza gharama lakini pia uhakika kuepuka kutumia ndege za kawaida za abiria na kuwapa nafasi wenyeji wao kupanga mipango ya kuiangamiza.

Yanga inashuka dimbani dhidi ya Plutinum Jumamosi ikiwa ugenini baada ya kushinda mabao 5-1 katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.

“Kweli, uongozi wa juu unaendelea kushughulikia suala la safari na tayari upande wa serikali umekubali kuikodisha ndege yetu,” kilieleza chanzo cha uhakika.


Yanga inahitaji sare ya aina yoyote ili kusonga mbele na ikifanikiwa itakutana kati ya Etoile du Sahel ya Tunisia au Benfica kutoka Angola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic