April 18, 2015

KAVUMBAGU (KULIA) WAKATI AKIWA YANGA.
Beki wa kati wa zamani wa Simba, Said Kokoo, amesema timu sahihi inayomfaa straika wa Azam, Didier Kavumbagu ni Yanga na si vinginevyo.

KOKOO (KUSHOTO) WAKATI AKIWA MORO UNITED.

Kwa sasa Kavumbagu amebakiza siku chache katika mkataba wake wa mwaka mmoja na Azam na tayari yupo katika mazungumzo na uongozi wa Yanga ili aweze kurejea klabuni hapo.

Kokoo ambaye ni raia wa Burundi na rafiki wa karibu wa Kavumbagu, amesema kuwa, kama mchezaji huyo anataka mafanikio, basi aende Yanga.

“Mimi ndiye niliyemshauri Kavumbagu ajiunge na Azam baada ya Yanga kukaa kimya kuhusu mkataba wake mpya, lakini sasa mambo si mazuri Azam na Yanga ndiyo mahali pazuri kwake kucheza soka,” alisema Kokoo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic