April 2, 2015


Ishu ya beki Hassan Kessy ameamua kujiondoa katika kambi ya Simba.


Kessy ameondoka kambini kwa madai ya kutotimiziwa fedha zake Sh milioni 15 anazoidai Simba. Tayari yuko nyumbani kwao Morogoro huku Simba ikitua mjini Shinyanga kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Kagera.

Lakini kumekuwa na hali ya kuchanganya huku uongozi wa Simba nao ukijitetea kwamba suala hilo liko katika mchakato.

"Kila kitu kilikuwa kinakwenda vizuri na kipo katika mchakato," alisema mmoja wa viongozi wa Simba.

"Lakini ajabu, Kessy kaamua kuondoka tu. Sasa sisi tunachukulia kama ni utovu wa nidhamu," alisema.

Kwa upande wa Kessy yeye alisisitiza kwamba Simba wamemfanya aishi kama ndege.

"Niliahidiwa nyumba, hadi sasa sina pa kuishi. Mimi kwetu Morogoro, sasa siwezi kuishi Dar kama ndege, leo niko hapa, kesho kule," alisema.

Simba imemsajili Kessy kutoka Mtibwa Sugar na amekuwa akionyesha kiwango kizuri katika beki ya kulia.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic