April 18, 2015




MPIRA UMEKWISHA
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Baghdad analambwa kadi ya njano baada ya kujiangusha.

Dk 89 Kom analambwa kadi ya njano kwa kumchezea madhambi Niyonzima
Dk 83, Tambwe anaifungia Yanga, lakini mwamuzi wa akiba anasema alikuwa ameotea

Dk 81, Yanga wanamtoa Juma Abdul aliyeumia na nafasi yake inachukuliwa na Rajab Zahir.

Dk 80, Niyonzima anawatoka mabeki na kupiga shuti kali lakini kipa analala na kudaka kwa ustadi mkubwa

Dk 79, Tambwe anapiga shuti kali baada ya kumtoka beki kipa anadaka
Dk 77, Yanga wanamtoa Hassan Dilunga na nafasi yake inachukuliwa na Kpah Sherman

Dk 76 Rami analimwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Tambwe


Dk 73, Yanga wanafanya shambulizi jingine kali lakini mpira wa kichwa wa Tambwe unaokolewa na kipa

Dk 66, Yanga wanaendelea kucheza kwa uoga utafikiri wao ndiyo wako ugenini.
Dk 62, Baghdad yeye na Barthez kwa mara nyingine lakini anapaisha juuuuu

Dk 60, shambuilizi kali la Yanga kipindi cha pili, Ngassa anampa Msuva pasi nzuri lakini shuti lake linaokolewa na kipa kwa ustadi mkubwa.

Dk 54, Brigui anatolewa na nafasi yake inashukuliwa na Tej
Dk 53 Brigui analambwa kadi kwa kupoteza muda

Dk 51 Msuva anapata pasi nzuri ya Niyonzima ndani ya eneo la hatari lakini anashindwa kufunga

GOOOOOOOO Dk 47, Ben Amour Amine anafunga bao baada ya kupiga shuti kali la chini linalomshinda kipa Barthez na kutinga wavuni.


Dk 46, Yanga inamtoa Cannavaro aliyeumia na nafasi yakeinachukuliwa na Said Juma Makapu.

********** DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45 shambulizi jingine katika lango la Yanga, Barthez anaokoa
Dk 44, shambulizi na Yondani anapiga shuti kali na mpira unapaa
Dk 39, Cannavaro anaokoa na kuwa kona, wasshambulia Etoile wanashambulia na kupata kona nyingine.

Dk 35 Etoile wanakosa bao la wazi, mara nyingine wanashambulia na Barthez anaokoa.

 Dk 30 Yanga wanashambuliwa zaidi, wao wanaonekana kutojiamini huku safu yao ya kiungo ikiwa imekufa kutokana na Hassan Dilunga kupotea katika mambo mawili. Kwanza ukabaji na pili uendeshaji wa timu.


Dk 29, Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali la Amine, ameumia na anatibiwa.
Dk 26 Bedui Rami anapata nafasi nzuri lakini anapiga kichwa dhaifu kinachodakwa na Barthez

KADI YA NJANO Dk 24 Niyonzima analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo.

Dk 22 Bado inaonekana Etoile ndiyo wanaocheza kwa kujiamini zaidi ukilinganisha na Yanga kwa kucheza pasi za karibu na mipira mirefu kushitukiza.

Dk 20, krosi nyingine nzuri langoni mwa Yanga, Baghadad anajaribu kufunga lakini Cannavaro anaokoa.

Dk 15, Naguez Hamdi akiwa katika nafasi nzuri anashindwa kufungwa. Etoile wanaendelea kushambulia zaidi.

Dk 12, krosi nyingine ndani ya lango la Yanga, kazi nzuri ya Yondani anaokoa na Barthez anadaka. Hadi sasaYanga haijafanya mashambulizi kwa dakika tatu, huku Etoile wakifika zaidi langoni


Dk 8, Baghdad anaingia ndani ya eneo la hatari, anapiga shuti linalompita Barthez lakini Yondani anaokoa kabla haujavuka mstari.


Dk 5 Pamoja na kufungwa, Etoile wanaokana kucheza kwa kujiamini huku wakipanga mipango, Yanga wanakuwa kasi zaidi ya Etoile.


Dk 4 Alaya Brigui anapiga shuti kali lakini Barthez anadaka.
GOOOOOOOOO dk 2, Cannavaro anafunga vizuri na kuiandikia Yanga bao

PENAAAAAAT Dk 2, pasi nzuri ya Niyonzima, Msuva anaangushwa na kuwa penalti

Dk ya kwanza Yanga wanapata kona, lakini Etoile wanaokoa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic