April 19, 2015


Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema Etoile du Sahel waliwachanganya kwa kushambulia mfululizo wakati wao walitegemea tofauti.


Mechi hiyo ya kwanza ya Kombe la Shirikisho hatua ya raundi ya pili ilimalizika kwa sare ya mabao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.

Akizungumza kuhusiana na mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Shirikisho, Mkwasa alisema waliamini watajilinda sana na wao watashambulia, lakini ilikuwa tofauti.

"Walituharibia mipango yetu, utaona kipindi cha kwanza waliweza kuwa bora zaidi. Lakini tulivyorudi vyumbani tuliweza kubadili mambo.

"Tulicheza vizuri zaidi katika kipindi cha pili na utaona tulitengeneza nafasi zaidi lakini hatukuwa na bahati.

"Sisi bado tuna matumaini na tunaendelea na maandalizi ili kujiweka sawa, lengo likiwa ni kushinda," alisema Mkwasa.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic