April 27, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameonya kuwa si sahihi kwa wachezaji wake kuungana kwenye sherehe za ubingwa kabla ya kuishinda Polisi Moro, leo.


Yanga inaikaribisha Polisi Moro katika mechi ya Ligi Kuu Bara, iwapo itashinda, basi itakuwa imejihakikishia kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara unaoshikiliwa na Azam FC.

Pluijm amesema mashabiki wana kila sababu ya kuanza sherehe kwa kuwa ni furaha ya. Lakini wachezaji wana deni kubwa la kuhakikisha wanatimiza ndoto yao.

“Mechi haitakuwa lahisi kwa kuwa Polisi wako mkiani, sisi tuko kileleni. Kila mmoja ana vita yake, anataka kushinda.
“Kazi yetu ni kucheza na kuhakikisha tunafanya vizuri, nimezungumza na wachezaji na nitaendelea kusisitiza kabla ya mechi,” alisema.


Yanga imekaa kileleni ikiwa na pointi 52, ikishinda leo itafikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC ambayo ikishinda mechi zake zote tatu itakuwa na pointi 54.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic