April 17, 2015


Klabu ya Simba imesisitiza inataka kushinda mchezo wake wa kesho dhidi ya Mbeya City.

Simba wamesema mchezo huo wameuweka kwenye programu ya mechi zao tano za ushindi ambazo zitawapatia pointi 15 zitakazowawezesha kushika nafasi ya pili.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema Simba imejiandaa vizuri licha ya kutokuwa na mshambuliaji wake Emmanuel Okwi.

“Tunajua Mbeya City wana timu nzuri lakini hiyo haiwezi kutuzuia kuendelea na mpango wetu wa kushinda mechi tano kwa ajili ya kupata pointi kumi na tano.
“Niamini, Mbeya City wako kwao lakini hawawezi kukwepa kipigo. Hilo halina mjadala,” alisema Manara.


Tayari Simba imetua mjini Mbeya kujiandaa na mechi hiyo ambayo Mbeya City pia wanahitaji kushinda ili kuendelea kujiweka vizuri na kuondoka katika mwendo wa kusuasua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic