April 1, 2015



Kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho hatakwenda Zimbabwe kuipigania timu yake ya Yanga ikipambana na FC Platinum katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho, kikosi kizima kinatarajia kuondoka kesho.


Pamoja na Coutinho, Jerry Tegete pia hatakwenda kwa kuwa majeruhi kama ilivyo kwa Mbrazili huyo.

Lakini Daktari wa Yanga, Juma Sufiani amesema wanafanya juhudi mshambuliaji Mliberia, Kpah Sherman, aungane nao.

"Tegete na Coutinho inaonekana hawataweza. Lakini tunaangalia kuhusiana na Sherman, hali yake ikiwa vizuri anaweza akaungana na kikosi kwenda Zimbabwe," alisema Sufiani.

Yanga inakwenda kupambana na Wazimbabwe hao baada ya kuwachapa kwa mabao 5-1 jijini Dar es Salaam.

Tegete na Sherman walikuwa fiti, lakini Coutinho anakwenda takribani wiki ya nne bila ya kucheza baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Mbeya City.

Hali iliyosababishwa Yanga imuache katika safari ya kwenda Botswana kuivaa BDF XI.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic