April 18, 2015



Uongozi wa Yanga umeendelea kusisitiza kuchukua mamilioni ya Azam TV ili waonyeshe mchezo wao dhidi ya Etoile du Sahel leo.


Yanga inaivaa Etoile kutoka Tunisia na mechi hiyo haitaonyeshwa. Kwani hata baada ya Yanga kukataa awali, Azam TV iliendelea na juhudi kutaka kuonyesha mechi hiyo kwa mara nyingine au baada ya mechi, bado ikashindikana kutokana na msimamo wa Yanga.

Azam FC ilikubali kutoa hadi milioni 20 ili mechi ionyeshwe baada ya kucheza, Yanga ikasisitiza Sh milioni 50.

“Kweli Azam FC wameshindwa, sisi tumeona ni bora kiasi tulichowaambia, imeshindikana basi,” alieleza mmoja wa viongozi wa Yanga.


Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic