April 29, 2015

CHACHA AKIELEZEA KUHUSIANA NA GAZETI LA DIMBA....
Uongozi wa Yanga ambao ni mabingwa wapya wa Tanzania Bara umetangaza kufungua kesi ya madai dhidi ya gazeti la Dimba ukitaka kulipwa fidia ya bilioni 3.

Yanga inataka kulipwa fedha hizo kufidia usumbufu mkubwa ilioupata baada ya gazeti hilo katika toleo lake la leo Aprili 29 namba ISSN 0856-2698 lililoandika kichwa kikubwa cha habari “Manji kufuru Yanga.”

Sehemu ya stori hiyo kubwa ilikuwa ikielezea uamuzi wa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kutoa nyumba na magari kwa wachezaji wake.

Mwanasheria wa Yanga, Frank Chacha amezikanusha habari hizo na kusisitizi hakuna chochote kuhusiana na suala hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Yanga jijini Dar es Saaam leo, Chacha amesema gazeti hilo limekuwa likiwanukuu vibaya au kunukuu ambacho hajasema viongozi wa klabu hiyo.

“Mara kadhaa, hali hii imekuwa ikitokea. Magazeti kadhaa ya nyuma pia yamefanya hivyo (alisema huku akionyesha baadhi ya magazeti ya Dimba).

“Hatuoni kama hili ni sahihi, hivyo pia tunawazuia Dimba kuandika habari zetu hadi hapo watakapoanza kuziandika kwa usafaha,” alisisitiza Chacha.


Hata hivyo, alisisitiza Yanga wanahitaji ushirikiano kutoka kwa vyombo vya habari huku akiamini kilichofanywa na Dimba hakikuwa sahihi na kinalenga kuvuruga umoja wa Yanga na Wanayanga kwa ujumla.

1 COMMENTS:

  1. Tatizo magazeti yetu ysmekuwa ya udaku, na sio dimba tu wapo wengi hata kwenye hizi blog wanaandika habari za kusadikika na vijiweni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic