May 5, 2015

Manny Pacquiao anatarajia kufanyiwa upasuaji wa bega lake ikiwa ni siku chache tu baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.


Imeelezwa kuwa bondia alipambana na Mayweather huku akiwa na maumivu makali ya bega.

Lakini majibu ya kipimo cha MRI baada ya pambano hilo, yameonyesha kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji.

Taarifa nyingine zimeeleza kuwa Pacquiao  alikataliwa kuchoma sindano ya maumivu kabla ya pambano hilo.


Pia baadhi ya habari zimeeleza kwamba bondia huyo alikosa siku kadhaa za mazoezi kutokana na hali hiyo ya maumivu wakati akijiandaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic