May 6, 2015


Mashabiki wengi wikiendi iliyopita walishtushwa kuona beki kisiki wa Azam FC, Pascal Serge Wawa akitolewa kipindi cha pili cha mchezo huo wakati yeye ndiye nguzo ya Azam, lakini imebainika kuwa alicheza mechi hiyo dhidi ya Simba akiwa anaumwa Malaria.


Wawa raia wa Ivory Coast, alifanikiwa kumdhibiti Emmanuel Okwi lakini baadaye nafasi yake ilichukuliwa na kiungo, Mudathir Yahya.

Kuhusu suala hilo, Kocha Mkuu wa Azam, George ‘Best’ Nsimbe alisema: “Sikuwa na jinsi, ilibidi tumtoe Wawa baada ya kusema hawezi kuendelea, najua alikuwa akisumbuliwa na malaria jana (Jumamosi), lakini asubuhi alisema yupo fiti ndiyo maana nikampanga.”

Hata hivyo, jana Jumanne Daktari wa Azam, Mbarouk Mlinga, alisema Wawa anaendelea vizuri na anaweza kuwepo kwenye mechi hizi mbili zilizosalia ikiwemo ya leo dhidi ya Yanga

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic