May 31, 2015


Mtanzania Francis Cheka amefanikiwa kumtwanga Mthailand, Kiatchai Singwancha kutoka Thailand katika pambano lililo la ubingwa.


Cheka ameshinda kwa Technical Knockout (KO) baada ya Singwacha kushindwa kuendelea na pambano katika raundi ya nane.

Mara baada ya kwisha kwa raundi ya saba, Singwacha alitangaza kushindwa kuendelea na raundi ya nane, hivyo kufanya Cheka kupata ushindi huo wa KO.,

Tokea mwanzo, Cheka kutoka Morogoro, alionekana kuwa makini zaidi huku akipiga ngumi za kuvizia.


Cheka ambaye ametoka jela na hili ni pambano lake la kwanza alizidi kumpa wakati mgumu Mthai huyo kila raundi zilivyokuwa zikiongezeka hadi aliposalimu amri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic