May 27, 2015


Bondia Mtanzania, Francis Cheka, anatarajia kuwasili jijini Dar leo Jumatano akitokea mkoani Morogoro ambapo alikuwa akifanya mazoezi ya kujiandaa na pambano lake dhidi ya Mthailand, Kitschai Singwacha litakalofanyika Jumamosi ya wiki hii kwenye Ukumbi wa Sabasaba PTA, Dar.


Huku Cheka akitarajiwa kuwasili leo, mpinzani wake anatarajiwa kuwasili kesho Alhamisi mchana ambapo mbali na pambano hilo la raundi kumi, mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo ni Kasim Ouma kutoka Marekani ambaye atapigana na Mtanzania, Shaban Kaoneka, huku Mtanzania mwingine, Cosmas Cheka akidundana na Mkenya, Fred Nyakes.

“Ninatarajia kuingia jijini Dar Jumatano (leo) tayari kwa pambano hilo ambalo nina imani nitaibuka na ushindi kutokana na maandalizi niliyoyafanya,” alisema Cheka.
Pambano hili la kihistoria, limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers, Pepsi na Fore Plan Clinic.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic