May 28, 2015

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemtaka kiungo wao, Ramadhani Singano ‘Messi’ apeleke kopi ya mkataba ili kumaliza ubishi.


Hans Poppe amemtaka Singano kufanya hivyo ili kupunguza kelele zinazoendelea sasa.


Singano amekuwa akilalamika kwamba Simba wamecheza mchezo na kumuongezea mwaka mmoja kwenye mkataba wake ulio TFF.

Lakini Hans Poppe amesisitiza mkataba wa Messi unamalizika mwakani na si mwaka huu kama ambavyo amekuwa akisema kiungo huyo.

“Yeye alete mkataba tu, kawaida kunakuwa na kopi tatu. Yake, yetu na ya TFF. Sasa alete yake, sisi tutoe ili kuangalia wapi kuna tatizo.


“Nafikiri haitakuwa busara hili suala kuendelea kukuzwa wakati kulimaliza ni lahisi na mikataba yote ipo,” alisema Hans Poppe.

Hata hivyo, Hans Poppe alisisitiza kwamba anachotakiwa Messi ni kuwasilisha mkataba orijino na si kopi.

"Kopi mtu anaweza kuichezea, hivyo hatutakubali. Alete ule orijino kama ambavyo sisi tutafanya," alisema.

1 COMMENTS:

  1. Msaidieni Messi kwa ushauri unaofaa! Hata kama halipwi pesa ya pango mimi sioni kama ni sahihi yeye kuendelea kuishi katika maisha duni kama hayo! Mlinzi wa kampuni binafsi na mshahara wa 80,000/- anapanga na kuendesha maisha, sembuse yeye! wachezaji wetu wanatia aibu! mshahara anaopata hata uwe wa laki Tano bado hatakiwi kuishi hivyo inabidi ajitambue, nanyi waandishi wasaidieni hawa watoto kujitambua,vinginevyo mtawamaliza! Ina maana leo akikoma kucheza mpira kwa tatizo lolote ndo anakufa maskini kwa kushindwa kujipanga!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic