May 26, 2015

CHANONGO AKIWA NA WACHEZAJI WA STAND.

Uongozi wa Yanga, sasa umeamua kuimaliza ishu ya  kiungo Haruna Chanongo kwa kusema, imeachana naye kabisa.

Msimu uliopita, Chanongo aliichezea Stand United kwa mkopo akitokea Simba ambayo iliamua kumshusha ikidai hakuwa na kiwango kizuri.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema wameachana naye.
“Kweli tumeamua kuachana kabisa na Chanongo, sasa tunaendelea na taratibu nyingine,” alisema.

Dk Tiboroha alisema walikuwa kweli katika mazungumzo na Chanongo, lakini inaonekana kuna mambo kadhaa yameshindikana.

Amesema kutokana na mambo hayo kushindikana, basi wao wataendelea na mambo mengine na Chanongo wanamuacha aendelee na yake.

Habari za ndani kutoka ndani ya Yanga, zimeeleza kuwa walikuwa wamefikia makubaliano na Chanongo lakini baadaye akabadilika na kutaka fedha zaidi.

“Alitaka fedha, akakubaliwa. Kabla ya kusaini, ghafla akabadili tena na kutaka zaidi,” kilieleza chanzo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic