May 7, 2015

Wakati blog ya SALEHJEMBE ilivyoandika kwa mara ya kwanza kwamba Mrisho Ngassa alikuwa anaondoka nchini baada ya kujiunga na Platinum Stars ya Afrika Kusini, ilikuwa shida.


Kwa upande wa magazeti, lile kubwa zaidi la michezo la Championi nalo liliandika kuhusiana na mchezaji huyo kuwa anaondoka.

Baadhi ya blog zilikanusha kabisa zikionyesha kusisitiza kwamba kiungo huyo hakuwa anaondoka.

Ingawa Ngassa hakukanusha, bado blog hizo zilionyesha kupinga utafikiri ni wasemaji wa Ngassa.

Lakini jana, mara baada ya mechi ya Azam FC, Ngassa alizunguka akiwaaga mashabiki wa Yanga huku akiwa na ujumbe wa kuwashukuru.

Hiyo ilikuwa ni uthibitisho tosha kwamba Ngassa sasa amethibitisha kuwa anaondoka nchini kwenda kukipiga au kuendelea kusaka maisha.

KILA LA KHERI NGASSA KAMA UKIFANIKIWA KUONDOKA.


1 COMMENTS:

  1. Kila la kheri,tumeona juhudi zako na kweli unaipenda Yanga maana unaiacha Yanga pazuri.Mungu akubariki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic