May 4, 2015

MURO
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro amesema kuwa mkuu wa kitengo kama chake upande wa Simba, Haji Manara ameangukiwa na jumba bovu.


Muro amesema hayo akisisitiza kauli ya kwamba Simba haijafanya vizuri lakini Manara amekuwa akiendelea kusema maneno mengi.

Akizungumza mara tu baada ya kurejea akitokea Tunisia alipoongozana na kikosi cha Yanga, Muro alisema Manara amekuwa na maneno mengi wakati akijua Simba haina lolote msimu huu.

“Naye anazungumza sana, anajua jumba bovu limemuangukia. Lakini anazuga tu,” alisema.
MANARA
“Kuhusiana na suala la Yanga iifunge Azam kwa ajili ya kuisaidia Simba, hilo ni suala la klabu na kesho tutalitolea ufafanuzi.

“Tumeamua kufanya mkutano na waandishi kuzungumzia masuala kadhaa ikiwemo safari yetu ya Tunisia. Lakini hilo pia tutalitolea ufafanuzi,” alisisitiza Muro.


Yanga imetolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa bao 1-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia. Hivyo kuwa imeng’oka kwa jumla ya mabao 2-1.

3 COMMENTS:

  1. Msipange matokeo waziwazi nyie YANGA.

    ReplyDelete
  2. 1.YANGA
    2.AZAM
    Simba wasubiri kwanza,wajifunze ubinadamu.

    ReplyDelete
  3. Uwezo wa kumfunga Azam sisi Yanga hatuna. Kwanza wana machungu ya kufungwa na simba, pili wanahitaji ushindi ili kuipata hiyo nafasi ya pili lakini muhimu zaidi Yanga morali yetu ipo chini sana baada ya kufungwa Tunisia na Simba kutuzomea sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic