May 5, 2015


Ingawa watu waliidharau Juventus, lakini imeanza mechi yake ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwatuliza Real Madrid kwa kuwachapa 2-1.


Madrid ikiwa ugenini ilijikuta ikifungwa bao kupitia Alvaro Morata kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Madrid.

Lakini shujaa wa Juventus alikuwa ni Carlos Tevez aliyefunga bao la pili katika kipindi cha pili kwa mkwaju wa penalti.

Madrid walijaribu kujitutumua lakini hawakuweza kusawazisha, hali inayowalazimu kuwa na kazi ngumu katika mechi ya marudiano kwao Santiago Benabeu.

Kesho Barcelona watakuwa na kazi ngumu dhidi ya Bayern Munich.










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic