May 29, 2015



Kiungo mpya wa Yanga, Deus Kaseke ameongezwa katika kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa kuivaa Misri.


Pamoja na Kaseke ambaye amejiunga Yanga kwa dau la Sh milioni 35 akitokea Yanga, wengine watatu wameongezwa na wote wameanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Wengine walioongezwa katika kikosi hicho ni kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed pia beki wa timu hiyo Andrew Vincent na kiungo wa Azam FC, Gardiel Michael.


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ambaye amekalia kuti kavu kutokana na kikosi chake kwenda mwendo wa kusua, ameamua kuimarisha kikosi chake na imeelezwa atafanya mchujo kabla ya kwenda Misri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic