May 27, 2015


Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa, ametamka kwa kujiamini kuwa, kama uongozi wao utafanya usajili kwa wachezaji waliowapendekeza kwenye ripoti, hakika timu za ligi kuu zitakiona cha moto.


Mkwasa ambaye anafanya kazi chini ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amesema walipendekeza wachezaji bora sana na anaamini kuwa wakipatikana wote basi watafanya vizuri kwenye ligi ambayo ina timu bora kama Simba, Azam na Mbeya City.

Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache tangu viongozi wa timu hiyo wafanikishe usajili wa kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Deus Kaseke aliyesaini mkataba wa miaka miwili.

Mkwasa alisema kuwa ripoti waliyoikabidhi kwa viongozi inaeleza kuwa wamelenga kufanya usajili bora wa kushiriki vyema Ligi ya Mabingwa Afrika na siyo ligi kuu tu ili kuhakikisha timu inafikia malengo.

 “Kama tuliweza kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika tulilotolewa na Etoile du Sahel, mwaka huu kwa kikosi kile tulichokuwa nacho, itashindikana vipi tushindwe kufika mbali katika Ligi ya Mabingwa tutakayoshiriki mwakani.

“Ninaamini katika michuano ya kimataifa ya mwakani tutafanya vizuri, tena katika kiwango kikubwa kutokana na ripoti ya usajili tuliyoikabidhi benchi la ufundi kwa viongozi wa kamati husika.


“Tumepanga kusajili wachezaji watakaotufikisha katika ‘levo’ za kimataifa, nawapongeza viongozi kwa kufanikisha usajili wa Kaseke ambaye yeye alikuwepo kwenye orodha ya wachezaji tuliowapendekeza,” alisema Mkwasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic