May 5, 2015


Kumbe hata Wazungu wanajua ile ishu ya “asui mwombee njaa!”. Maana Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesisitiza kwamba anatamani Azam iboronge michezo yote iliyobaki.


Kopunovic raia wa Serbia anaamini kama Simba itashinda mechi zote zilizobaki, Azam ikafulia, basi wao watabeba nafasi ya pili.

“Ndiyo, dua mbaya kwa mpinzani wako si vibaya. Si dua mbaya aumie, nazungumzie apoteze mechi,” alisema huku akitabasamu.

Simba iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 44, wakati Azam FC iko katika nafasi ya pili ikiwa na nafasi 45.
Kesho Azam FC inashuka dimbani kucheza na Yanga

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic