May 3, 2015


Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amesema wanapaswa kushinda mechi ya leo dhidi ya Azam FC.


Kopunovic amesema anaiona siku ya leo ni muhimu na maalum kwao kwa kuwa watapata dira kama wataweza kuwashinda Azam FC.
Simba inashuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuivaa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

“Tukishinda leo, angalau tunaweza kusema bado tuko katika mbio za kuwania nafasi ya pili.

“Kama tutapoteza, basi tutakuwa tumeondoka katika kuwania nafasi ya mshindi wa pili,” alisema.


Raia huyo wa Serbia amesema anakiamini kikosi chake kwamba kina uwezo wa kufanya vizuri na kuibuna na ushindi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic