May 2, 2015

Etoile wanafanya mabadiliko kupoteza muda
DAKIKA 90+3
Dk 84&88 Yanga wanaonekana kuwa fiti zaidi, wanashambulia kwa kasi huku Etoile wakiwa wamerudi nyuma kwa wingi.

SUB: Dk 83, Yanga wanamtoa Telela na nafasi yake inachukuliwa na Coutinho

Dk 81, Youssef tena anapata nafasi vizuri sana anapiga kichwa lakinianapaisha
Dk 78, Banghoura anaingia katika eneo la hatari anapiga vizuri lakini Dida anadaka safi kabisa
KADI Dk 72 Yondani analambwa kadi ya njano kutokana na kumfanyia madhambo Youssef
Dk 71, Dida anafanya kazi nzuri ya kudaka mashuti mawili mfululizo ya Waarabu

DK 70 Tambwe anapata nafasi nzuri kabisa lakini anapiga shuti dhaifu

KADI Dk 64 Yanga wanamtoa Sherman na nafasi yake inachukuliwa na Hussein Javu
Dk 55&58, Yanga wanaonekana kuumiliki vizuri mpira na kuwapa wakati mgumu Etoile lakini bado mpira unachezwa katikati ya uwanja.

Dk 51, anajaribu kupiga shuti lakini linaonekana ni nyanya kwa kipa
Dk 47, Etoile wanalazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa mpira unaotoka nje. Kama Sherman angeuwahi ingekuwa jambo jingine

Dk 45, Makapu anaokoa mpira uliompita Dida ukienda kuvuka msitari baada ya Youssef kuwatoka mabeki Juma Abdul na Yondani.

KADI Dk 42 Kom raia wa Cameroon analambwa kadi ya nyekundu kwa kumfanyia madhambi Msuva..anakwenda nje

Dk 33, Sherman anapoteza nafasi nzuri kabisa baada ya kupokea pasi nzuri ya Ngassa lakini anashindwa kuitumia kwa kupaisha buuu
Dk 30 Yanga wanafanya shambulizi kali, Ngassa anapiga krosi nzuri lakini Etoile wanaokoa na kuwa kona
GOOOOOOOO Dk 25 Ammar Jemal anaifungia Etoile bao la kichwa baada ya krosi nzuri ya Kom na difensi ya Yanga kupoteana.

Dk 24, Kom anapiga shuti kali  lakini Dida anaokoa na kuwa kona
Dk 21, Dida anaanguka baada ya kufanyiwa madhambi, mwamuzi anaruhusu atibiwe
KADI Dk 19, Tambwe analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo...Dk 18, Youssef Mohebi anageuka anageuka na kupiga shuti kali ndani ya eneo la hatari la Yanga, mpira unatoka nje kidogo.

Kwa upande wa Yanga, nahodha ni Mbuyu Twite katika mechi ya leo..
Mechi imeanza kwa kasi kubwa. Tayari Etoile wamefika mara tano langoni mwa Yanga na Yanga wakiwa wamefika mara mbili tu.

Mpira una kazi kubwa lakini Yanga wanaonekana kuihimili.
Hata hivyo Etoile wanatumia mipira ya kasi na krosi kutaka kufunga lakini kipa Deogratius Munish ‘Dida’ anakuwa makini.



2 COMMENTS:

  1. Tumecheza mpira mkubwa sana, kilichotuangusha ni game ya kwanza!! Kikosi kisibadilishwe

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic