May 28, 2015


Kundi maarufu  la vichekesho nchini la Olijino Komedi sasa limeamua kuingia kwa nguvu katika biashara ya kilimo.


Wasanii hao wamekabidhiwa Matrekta saba aina ya Sonalika DI 50 RX na Kampuni ya Quality Extended Enterprise ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilimo.

Baada ya kuyanunua, Orijino Komedi walikabidhiwa Mtrekta hayo yenye thamani ya Sh milioni 170  katika hafla iliyofanyika makao makuu ya Quality Extended Enterprise yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar.

Kiongozi wa Orijino Komedi, Sekioni David ‘Seki’  alisema kuwa hatua hiyo ni moja ya malengo yao ya kimaendelo waliyokuwa wamejiwekea  hapo hawali wakati walipokuwa wakianzisha kundi hilo.

Alisema malengo yao yalikuwa ni kuhakikisha wanafikiwa zaidi kimaisha lakini pia wanakuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine hapa nchini.

“Tulianzisha kundi hili siyo kwa ajili ya buradani pekee lakini pia kwa ajili ya maendeleo yetu binafsi hivyo baada ya kupata matrekta haya tutajikita rasimi katika kilimo.

“Tayari tumesha mashamba mkoani Mbeya na Iringa lakini pia tupo katika mazungumzo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Yusuf Makamba ili aweze kutupatia shamba jingine huko kwao mkoani Tanga ili tuweze kutimiza ndoto zetu,” alisema Siki.
 Kundi la Olijino Komedi linaundwa na wasaanii saba ambao ni Seki, Mpoki, Joti, Masanja, Wakuvanga, Macklegan pamoja na Vengu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic