May 25, 2015



Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm atarejea nchini Juni 6 tayari kuanza kazi.


Yanga imejipanga kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya Juni 8 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro amesema Pluijm raia wa Uholanzi, mara moja ataanza mazoezi na timu hiyo baada ya kurejea.

“Kocha kama mnavyojua yuko mapumziko, baada ya kurejea ataanza kazi moja kwa moja. Lengo ni kuanza maandalizi mapema kabisa,” alisema.

“Kuna michuano ya Kagame, pia kuna michuano mingine ya kimataifa pia ligi kuu, hivyo lazima tuanza maandalizi mapema.”


Yanga tayari imeanza kufanya usajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake ambacho pamoja na michuano ya Kagame, kitashiriki ligi ya Mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic