May 24, 2015

 Cristiano Ronaldo ni nomaaa, amepiga hat-trick nyingine wakati Real Madrid ikiichinja Getafe kwa mabao 7-3 katika mchezo wake wa mwisho wa La LiGa msimu huu.


Kwa mabao hayo Ronaldo amefikisha mabao 48 na kufanikiwa kubeba tuzo ya Pichichi ya mfungaji bora ambayo amekuwa akikimbizana na Lionel Messi wa Barcelona.

Kwake pia ni hat trick ya saba tokea ajiunge na Real Madrid akitokea Manchester United. Hivyo ana jumla ya mabao 61 kwa msimu mzima.
Kwa jumla ya mabao 61, Ronaldo amevunja rekodi yake ya awali ya mabao 60 kwa msimu wa 2011-12.

Raul anaendelea kuongoza kwa kuwa mfungaji bora zaidi Madrid kutokana na mabao yake 323 katika mechi 741 alizoichezea timu hiyo wakati Ronaldo ambaye tayari ameichezea Madrid mechi 300 amefikisha mabao 313 akiwa amebakiza mabao 10 tu kumng’oa Raul.










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic