May 5, 2015

 Simba imeendelea na mazoezi leo kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam kujiwinda na mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara.

Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema wanaendelea kupambana na wanachotaka ni kushinda mechi zilizobaki.
“Kwetu msimamo ni uleule, kupambana na kushinda mechi zilizobaki. Hayo mengine yatafuatia tutaona.
“Katika soka hautakiwi kukata tamaa, unashindwa mwisho kabisa na si sasa,” alisema Matola akionyesha kujiamini.

Simba walionekana na furaha na walifanya mazoezi ikiwemo kucheza soka.

Mazoezi yao yalikuwa makali utadhani ni mechi huku wachezaji wakikabana kwa nguvu “kijeshi”.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic