May 29, 2015


Simba imemsajili kipa namba moja wa Mohammed Abrahman Mohammed wa JKU.


Kipa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili leo mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ofisini kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.


Hans Poppe amesema wamemsajili kipa huyo kuimarisha safu yao ya ulinzi.

Ingawa hakuzungumzia lolote kuhusiana na wingi wa makipa, kutua kwa Mohammed, maana yake ni safari kwa kipa Hussein Shariff ‘Casillas’ ndiyo anaondoka Simba.

Mzanzibari huyo anafanya idadi ya makipa wa timu kubwa ya Simba kufikia wanne.
Pamoja na yeye ni Ivo Mapunda, Peter Manyika na Casillas ambaye inaonekana safari imemkuta.

,   

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic