May 27, 2015


Kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, leo Jumatano kinatarajia kuingia kambini jijini hapa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya ya Misri.


Kikosi hicho kinaingia kambini leo huku kukiwa na uteuzi mpya wa wachezaji ambao wameongezwa kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, alisema kuwa kikosi hicho kimeteuliwa na kocha Mart Nooij kuongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo ambacho kilikwenda nchini Afrika Kusini.

“Kocha Nooij ameamua kuteua kikosi cha wachezaji 16 ambao wataingia kambini Jumatano (leo) kwa ajili ya kuanza kujiwinda dhidi ya Misri.

“Kikosi hicho kimeitwa ili kukiongezea nguvu kile kilichoshiriki michuano ya Cosafa Afrika Kusini ambapo wachezaji wake wapo mapumzikoni, sasa baada ya hapo wachezaji wote wataungana Juni Mosi na kutengeneza timu ambayo itajiwinda kucheza michuano hiyo ya Afcon na Chan,” alisema Kizuguto.

Wachezaji ambao wameitwa katika kikosi hicho ni Jonas 
Mkude, Peter Manyika, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka (Simba), Salum Telela, Juma Abdul, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Aishi Manula, Mudathir Yahya, Frank Domayo na Kelvin Friday (Azam).

Wengine ni Rashid Mandawa, Atupele Green (Kagera Sugar), Haruna Chanongo (Stand United), Malimi Busungu (Mgambo JKT) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic