May 5, 2015

Binadamu tajiri kuliko wote barani Aliko Dangote amesema hajakata tamaa ya kuinunua klabu ya Arsenal.

Dangote raia wa Nigeria ambaye tayari ana kiwanda cha saruji mkoani Mtwara nchini Tanzania,  anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 10.4.
Tayari alitaka kununua shea za umiliki wa Arsenal wakati aliyekuwa mkurugenzi na mmoja wa wamiliki Lady Nina Bracewell-Smith alipoziuza mwaka 2010 lakini ikashindikana.

Lakini sasa Dangote amesisitiza yuko tayari na anataka kuwa mmoja wa wamiliki wa Arsenal.

Kwa sasa milionea wa Kimarekani, Stan Kroenke, ndiye mmiliki mkuu wa klabu hiyo.


Raia wa Uzbekistan, Alisher Usmanov naye anamiliki asilimia 30 za shea za klabu hiyo maarufu England na duniani kote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic