May 6, 2015


Wakati Klabu ya Simba ikilia na kipato kiduchu milangoni, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kushikilia mapato yao ya vyanzo vingine kuhakikisha zinapatikana shilingi milioni 22 za madai ya wachezaji wake wa zamani, Amissi Tambwe na Haruna Chanongo.


Chanongo anaidai Simba milioni 11.4 zilizotokana na kutolipwa mshahara wake akiwa kwa mkopo Stand United huku Tambwe anayekipiga Yanga kwa sasa anaidai dola 7,000 (milioni 11) kwa kusitishiwa mkataba.

Wiki iliyopita, TFF iliiagiza Simba kuhakikisha wachezaji hao wanalipwa kufikia Aprili 30, mwaka huu, vinginevyo watakatwa kwenye mapato ya mlangoni ili kupata kiasi hicho.

Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, amesema iwapo makato ya getini hayatatosha kufikisha kitita hicho, watalazimika kushikilia mapato ya vyanzo vingine ili kuhakikisha kabla ya ligi kufungwa wawe wamepata haki yao.

“Tayari tumeanza kukusanya malipo yao, Simba ilikatwa kwenye mapato ya mlangoni kwenye mchezo uliopita na Azam. Waligawana pasu kwa pasu, zilikatwa milioni tatu na timu ikachukua tatu,” alisema Kizuguto.


Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alikaririwa akisema kuwa timu hiyo kwa sasa imeyumba kiuchumi kutokana na mapato ya mlangoni kushuka kwa kiasi kikubwa kutokana na uchache wa watu viwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic